Raptor El Shariff - Mwezi Mwema lyrics

Published

0 260 0

Raptor El Shariff - Mwezi Mwema lyrics

Leo hii ni ya kwanza Tuwe wenye kujipinda Tufanye ano yapenda Na kumridhi jalia Tumuombeni jalali Mchana pia laili Na kila tunaposwali Atujaalie afia Tufunge bila usiri Tena kwa nyingi sururi Tupate yalo mazuri Mola ‘lotuandalia Tutieni moja nia Kuwa tutajifungia Kwa ikhlasi na nia Na unyenyekevu pia Nayo pia qurani Kwa hima tuisomeni Juzu tukamilisheni Japo mara wahidia Ni Ramadhani ya pili Tumuombeni jalali Atupe nasi sahali Tufunge bila udhia Maaswia tuacheni Kheri nyingi tufanyeni Usiku tuamkeni Ibada kujifanyia Tusipotezeni muda Kufanya yaso faida Bali tufanye ibada Hiyo ndio sawa ndia Ni mwezi wa kuyachuma Mambo mengi yalo mema Basi tufanyeni hima Thawabu kujipatia Pia tushikeni hamu Kuacha yalo haramu Kwani hini ni awamu Ya kutengea tabia Imewadia ya tatu Kuasi tusisubutu Tusafishe nyoyo zetu Tufuate sawa njia Tuchukueni sabuni Nyoyo zetu tuosheni Nyeupе tuzifanyeni Zitatengea tabia Tuwе sana wakarimu Daima tutabasamu Tupendaneni kaumu Na kuswafiana nia Pia sana tutoeni Tukumbuke masikini Toa japo ishirini Au hata moja mia Imewadia ya nne Mema tuamrishane Zaidi tuhimizane Maovu kuyakimbia Na mikono tushikane Pema tuelekezane Wengine tusitukane Na tukajiharibia Msaada tupeane Mazuri tuambiane Katu tusipotoshane Tukaja potea njia Enyi ndugu tupendane Tuloteta tupatane Usiku tuamshane Ibada kujifanyia Pia sana tung’ang’ane Ibadani tushindane Thawabu zipatikane Ziwe mia kwa mamia Leo tano Ramadhani Kamba tukaze jamani Tuzameni ibadani Thawabu kujichumia Tuleteni adhkari Usiku pia nahari Tuseme yalo mazuri Maovu kuyakimbia Darasa tusikilize Mambo mema tujifunze Katu damu tusilaze Mazuri kujifanyia Sadaka tutoe sana Vyema kusaidiana ‘tatubariki rabana ‘Kifuata sawa njia Ya sita imewasili Shukurani kwa jalali Kuzidi tupa sahali Saumu kujifungia Tuzidi sana kuswali Kwa ikhlasi ya kweli Maovu tuweke mbali Tuzidi kuyakimbia Pia swala za laili Tuamkeni tuswali Ndio mwendo wa rasuli Nao maswahaba pia Tufanye yalo mazuri Tena kwa hamu na ari Maovu tutahadhari Yasije tuharibia Ya sabaa imefika Kwa uwezo wa Rabuka Kamba tuzidi kushika Tusije iachilia Tusipoteze wakati Jikoni sana kuketi Kuzipika kaimati Na vyakula ainia Na sana tujitahidi Tuweze kuzifaidi Za Ramadhani zawadi Mola ‘lotuandalia Tusikubali kabisa Fadhla nyingi kuzikosa Hivyo tuache mikasa Itayotuharibia Ni ya nane Ramadhani Shukurani kwa manani Kututia uzimani Tuna siha na afia Fursa tuitumieni Kuzizidisha imani Na tujirekebisheni Ziwe nzuri tabia Miraa tuiacheni Sigara tusivuteni Nayo pombe tusinyweni Mchana usiku pia Tabia tuache nyuma Zile zisizo njema Tufuate mwendo mwema Mwendo wa wetu nabia Kwa uwezo wa Rahimu Ya tisia imetimu Tuifungeni saumu Kwa ilio safi nia Tupunguzeni kulala Tuamkeni laila Na kusimamisha swala Tutubuni sana pia Tuamkeni suhuri Karibu na alfajiri Ndio suna ya bashiri Tusiwe tutapuzia Ya kumi ni leo hii Basi tufanye bidii Mola tuzidi mtii Tusichoke nawambia Hakika ya mwezi huu Fadhila zipo ni kuu Tusije tukala huu Mema kutojifanyia Tufanye kwa kila hali Aturidhie jalali Na adhabu kali kali Mola ‘tatuepushia Tuzishindeni nafusi Tuyaepuke maasi Tumuombeni Qudusi Atuonye sawa ndia Kwa furaha tulianza Sasa kumi ‘memaliza Basi tusije legeza Kamba tukaachilia Leo ni kumi na moja Tujizatitini waja Ili tuone natija Mwishoni tukifikia Kwa wingi tukisomeni Kitabu chenye thamani Si kingine Qurani Nazidi kuhimizia Adhkari tusomeni Asubuhi na jioni Nyoyo ‘tapata amani Na pia kufurahia Shukurani kwa jalali ‘Mefika kumi na mbili Tuache lile na hili Tufunge kwa safi nia Kwa safi nia tufunge Pia vyema tujipange Mengi mema tuyachange Mizani kujijazia Ziwe nzito mizani Tufikapo hisabuni Mwisho tungie peponi Tukawe naye nabia Basi tufanyeni hima Tujitahidi kuchuma Mengi mengi yalo mema Sadaka na zaka pia Atujaalie Wahabu Qiyama ‘sipate tabu Tuvipokee vitabu Kwa mkono wa kulia Leo ni kumi na tatu Tusafishe nyoyo zetu Tuitoe yote kutu Turekebishe tabia Mwenendo uwe mzuri Tuzifanye nyingi kheri Adhabu zote na nari Mola ‘tatuepushia Tuzidisheni juhudi Tumuombeni Wadudi Sisi sote atuhidi Kwenye ilo sawa njia Kumi na nne yaumu Ndugu tushikane hamu Kuyaacha ya haramu Halali kukumbatia Tuifungeni saumu Kwenye ibada tudumu Tutapata ladha tamu Ya imani nawambia Tuweni na ikhlasi Riya tuseme ni basi Na malipo kwa Qudusi Tuwe tutatarajia Leo ni kumi na tano Tuyaache magombano Kutoleana maneno Na kutukanana pia Tusiweni tutateta Na kuvieneza vita Na kizazi kukita Hizo si njema tabia Tuishi kwa itifaki Tuzitoe zote chuki Upendo uwe wa haki Nyoyo zutafurahia Kumi na sita ‘mefika Tuzitengeze huluka Nazo Radhi za Rabuka Tuwe tutajipatia Mwenendo wake Hashima Kiigizo chetu chema Tufuate hima hima Hiyo ndiyo sawa njia

You need to sign in for commenting.
No comments yet.