One The Incredible - Haya Maisha lyrics

Published

0 647 0

One The Incredible - Haya Maisha lyrics

Intro; Yo, M-Lab, One Uh, Mujwahuki, Den Tex Yo, Cheki [Verse I: One The Incredible] Bado njaa uswahilini Napo kaa panatisha, mpaka nashangaa kuwa mimi Hapa hapa mjini bado kuna nyumba za udongo Mama hana mchongo mpaka ana amua auze gongo Ili dogo aende shule Nakule hakuna walimu, ina gharimu hela ndogo iende bure Utachanganyikiwa na maisha Hivi lini nami nitafanikiwa kuwa fisadi Watoto wasome bure, shule nzuri Huku dogodogo poa na mama watoto mzuri Vimada kila mtaa kisa hela Msela akishangaa sana mzigo, papaa namtupa jela Kula sana mali, ishi kifahari Ndani ya nyumba kubwa zaidi ya ofisi ya serikali Huku kwa maskini hali ni kheri Habari ya kweli, hatuna amani ya kweli Ibada zinashawishi masikini wajifilisi Ili kuwa tajirisha waajiri wa ibilisi Uswahilini ukichunguza, bado njaa Ni balaa, huyu Mungu wa Kakobe hana uchungu na mitaa [Hook: Songa] (Kamakawa si uchuni, bado zama ni duni Wahuni hawana maana washazama na uchumi Sijui nitafika au nitafichwa uvunguni Ama nitaishia njiani kama picha ya kubuni) x2 [Verse II: One The Incredible] Maarifa na mawaidha, faida ya afisa Nyadhifa ikishika, ni maafa ya taifa Pametanda giza, shida nchi imeota miiba Wananchi wananyata kimaisha Labda nitafika kwa imani Ila inatisha, siku hizi siasa imefika ibadani Nadhani zimeshafika nyakati Muda umewadia, hii dunia imeshafika tamati Sikia ujumbe, uwe mwenye nia safi Ulie kufikia, hakukufikia kwa bahati Utubu na ukumbuke Kwamba maisha magumu, inakubidi uwe sugu na usumbuke Uwakumbuke hata ndugu, usiwe bubu Wavute karibu, haitogharimu, usiwatupe Muumba nikumbushe, nikumbuke nielewe Nijapokuta jaribu, wa kumkumbuka ni wewe Nisamehewe napojuta kweli Ni wewe nakutukuza, naposumbuka kuitafuta kheri Ki ukweli yamenifika kwenye shingo Kilio cha mzawa kimesikika kwenye wimbo [Hook: Songa] (Kamakawa si uchuni, bado zama ni duni Wahuni hawana maana washazama na uchumi Sijui nitafika au nitafichwa uvunguni Ama nitaishia njiani kama picha ya kubuni) x4

You need to sign in for commenting.
No comments yet.