Alex Mwakideu - Mahaba haba (Shairi) lyrics

Published

0 273 0

Alex Mwakideu - Mahaba haba (Shairi) lyrics

Ni juzi tu tulipokutana Mimi na yule msichana Mkahawani tukapelekana Chai maandazi na mbaazi tukalishana Mapenzi yetu mbuga yakachana Na kwa mambo yote tukaelewana Ona sasa wataka kuwachana Na hata wazazi wetu hawajakutana Usinipeleke raba na mahaba yako haba Wakumbuka jumamosi ya tarehe saba Ile siku tulikutana saba saba Tukajivinjari kwa siku saba Wiki nzima hotelini katika kila chumba cha saba Malavidavi yakawa ni kwako tu habuba Zawadi nazo nikanunua tena zile babu kubwa Sasa nasema twende kwa baba kule malaba Kisha wasahau yangu yote mahaba Usinipeleke raba na mahaba yako haba Mwenzio nataka mapenzi ya kuaminiana Mimi na wewe kushikana Bega kwa bega tukiandamana Mungu akitujalia tupate na wana Moja kichuna aiitwe jina la mamako Ana Na mwingine kijana tumwite baba mzee chuna Sio tu kila siku starehe za gharama Na hali wewe mwenyewe hata peni huna Usinipeleke raba na mahaba yako haba Namalizia nikikusihi uwache pupa Usije ukayatupa mapenzi kwa pipa Utamu wa mapenzi ni kulipa Nikikupa na wewe wanipa Angani mwenzangu tutapaa Na chochote utakacho nitakupa Kwa hio tulia upate utamu hapa Hamna haja tena ya kutapa tapa Usinipeleke raba na mahaba yako haba Skiza albamu ya mahaba Na ujifunze mwenzangu habuba

You need to sign in for commenting.
No comments yet.